Tafakari
ya wiki hii ya Kwaresma tunakumbuka maisha ya Mama yetu Anna Michaeli Kinunda aka
Mbuya; tunayakumbuka maneno ya Yesu tukisoma Yohana 19:27 kisha akamwambia yule
Mwananfunzi ;Tazama Mama Yako;Je kunasiri gani Yesu alikuwa akimwonyesha yule
Mwanafunzi: Nguvu ya akina mama katika misha yetu ni kubwa sana. Upendo wao
hauna mipaka;
Leo
tunajikumbusha maisha ya mama Anna Kinunda (Mbuya) ambaye Mwenyezi Mungu
alimwita katika makao yake ya milele tarehe 13 December 2016. Mama ambaye
alikuwa amejaa furaha na Amani ya Bwana ukiondoa ubinadamu wetu ambao ni zao la
kila mmoja wetu; Mama Anna alikuwa Mtu mwenye nia thabiti juu ya Mungu wake;
alimtumikia Mungu kwa moyo wake wote na hakukatishwa tama na mtu au kitu
chochote alisimamia kile ambacho alikuwa anakiamini; Pamoja na ukweli kuwa kifo
kamwe hakizoeleki daima kinageuka kuwa ni jambo la kutisha na ambalo
halizoeleki; Mama Anna alikuwa tayari kwa kifo chake na alikisubiri na
kukipokea kwa unyenyeku siku ya jumatano tarehe 13 december huku akiwa
akiendelea na sala zake katika kumshukuru Mungu; alikutwa akiwa amepiga magoti
huku akiwa amefunga mikono yake katika ibada yake na Mungu wake; hivyo alikufa
katika unyenyekevu; na furaha kubwa;
Tukisoma kitabu cha wakorinto 2 : 5 : 1-5 hofu na woga
mkubwa sana ambao hugusa mioyo ya binadamu ni woga wa kifo; kifo kinatujengea
woga wa kiwango cha juu katika maisha ya binadamu kuliko woga wa kitu
kingine chochote. Tunaogoapa kufa; tunaogopa kifo pamoja na mafundisho
yote ya ahadi zilizo jaa faraja ambazo tumeandaliwa baada ya Kifo; bado
tumekuwa wagumu kukipokea kifo kwa unyenyekevu; bado tunakuwa na mashaka juu ya
kifo; tunakuwa na imani haba na kuamini kuwa hatujui nini kitatokea baada
ya kifo; kifo kimekuwa ni tatizo la msingi sana katika maisha ya binadamu; hata
wachungaji ambao wamekuwa wakihubiri kuhusu maisha yetu ya kifo ni mbinguni na
yatakuwa maisha yaliyojaa furaha lakini nao wanaogopa sana kifo ; Ili
tufurashie hiyo furaha ya milele lazima tufe na kifo ndio njia pekee ya
kutupeleka Mbinguni lakini sio njia ambayo tuko tayari kuipokea ; Mama yetu
Anna alikipokea kwa upendo mkubwa bila woga na alikisubiri bila mashaka
yeyote.
Tukisoma kitabu cha Yakobo 4:14 14 kinatukumbusha kwa
ufupi walakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni
mvuke uonekanao kwa kitambo, kisha hutoweka. Na mzaburi 90:5-6 naye
anatukumbusha kuwa Wawagharikisha, huwa kama usingizi, Asubuhi huwa kama
majani yameayo. 6 Asubuhi yachipuka
na kumea, Jioni yakatika na kukauka.
Kama
ilivyoelezwa katika mazingira tofauti kuwa hakuna kitu cha uhakika zaidi ya
kifo, na hakuna ambaye anaweza kukwepa kifo “ Kwa kila jambo kuna majira yake,
Na wakati kwa kila kusudi chini ya mbingu. Wakati
wa kuzaliwa, na wakati wa kufa;” Lakini tukisoma 2 Wakorinto 5: 1-2 Kwa maana
twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo
jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele
mbinguni. 2 Maana katika
nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni;
maandiko haya ya Paulo kwa wakorinto tunaelewa nini kipo mbele yetu, ukweli
wote ambao uko mbele yetu, matumaiani pamoja na mtafaruku wote wa kifo.
Tukumbuke kwa Mungu alishatowekea ushuhuda ambao hata kifo chenyewe hakiwezi
vunja. Wafilipi 1:21 Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni
faida.
Tukiamini katika imani tunagundua kuwa tunapokuwa katika khali ya
kifo ni tendo lenye umuhimu mkubwa katika maisha ya binadamu ukilinganisha ni
viumbe vingine vyovyote; tendo la viumbe au mimea kufa linakuwa limekamilika na
kufikia mwisho wake; lakini kwetu sisi
kama binadamu tunapoteza tu uwezo wa kutambua kibinadamu, hatuhisi chochote
kulingana na ubinadamu tuliokuwa tumeuzoea; na tunakuwa hatuko tena katika
ulimwengu huu wa kidunia lakini sasa maisha yetu ya kiroho yananza kulingana na
matendo yetu hapa duniani. Hatuishi kwa ajili yetu wenyewe bali maisha yetu
yanakuwa katika daraja jipya; ni maisha ya
kumsifu na kumshangilia Mungu siku zote; ndio wale ambao tunawashangilia
kuwa wamemaliza kazi katika utukufu wa Kimungu. Maisha yao yote na malengo
katika maisha yao ni kuishi katika utukufu wa Kimungu. Ndio wale ambao
wananungana na Mtume Paulo aliposema Warumi 14: 7-8 Kwa
sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa
nafsi yake. 8 Kwa maana kama
tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama
tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
Yesu katika mafundisho yake
alikuwa akisisitiza sana matendo mema; Imani ili iweze kufanya kazi yake
inahitaji matendo. Imani bila matendo hakuna wokovu. Tunaamini kuwa kila
muumini ambaye anaamini na anaishi kulingana na maagizo ya Mwenyezi Mungu
amekombolewa katika dimbwi la dhambi;
Mama
Anna alikuwa ni mwanamke aliyejaa matendo mema na kwa sadaka alizozitoa. 1
Timoteo 7-9 Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na
kitu; 8 ila tukiwa na
chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo. 9 Lakini
hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi
zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na
uharibifu. Mathayo 6:26-27 Kwa kuwa mtu atakaye kuiokoa nafsi yake,
ataipoteza; na mtu atakayepoteza nafsi yake kwa ajili yangu, ataiona. 26 Kwani atafaidiwa
nini mtu akiupata ulimwengu wote, na kupata hasara ya nafsi yake? Au mtu atatoa
nini badala ya nafsi yake?
Tunafundishwa
kuwa hatutakiwi kusoneneka kwa kukosa thawabu za Kimungu kwa matendo yetu
mabaya Yuda alisikitika kwa kumsaliti Yesu kwa vipande 30 vya Pesa; je wewe
kabal ya kifo chako unahuzunika kwa jambo gani? Je matendo yako yanakupa njia
sahihi ya Kufurahia utukufu wa Mungu? Je baada ya kifo wapendwa wako utawaacha
katika khali gani ya furaha au unyonge kufuatia maisha na matendo yako?
Mama Anna daima alikuwa akisema kuwa nimemaliza kazi na maisha
yangu kama Mkristo, nimetimiza wajibu wangu na nimewaonyesha njia kama Mkristo,
na sasa niko tayari kwenda kupumzika kwa Baba. Hakuwa na mashaka wala woga wa
kufa kwani alikuwa akiendelea kujiandaa kila siku na kuomba huduma za kiroho
kila siku. Kwake kila siku mpya ilikuwa ni siku ya Maombi. Daima alikuwa
akijiuliza mimi ni nani? Kwa nini mimi nimezaliwa? Na ninakwenda wapi? Je
nimetimiza majukumu yangu kama Mkristo?
Zaburi ya 37:28-29 Kwa kuwa Bwana hupenda haki, Wala hawaachi
watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa. 29 Wenye haki
watairithi nchi, Nao watakaa humo milele.
Mithali
3: 12 Kwa kuwa Bwana ampendaye humrudi, Kama vile baba mwanawe
ampendezaye. 13 Heri mtu yule
aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu. 14 Maana biashara
yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu
safi. 15 Yeye ana thamani
kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye. 16 Ana wingi wa siku
katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa
kushoto. 17 Njia zake ni njia
za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani. 18 Yeye ni mti wa
uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu ashikamanaye naye.
Mithali 16: 6-7 Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha
Bwana watu hujiepusha na maovu. 7 Njia za mtu
zikimpendeza Bwana, Hata adui zake huwapatanisha naye. 8 Afadhali mali
kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. 9 Moyo wa mtu
huifikiri njia yake; Bali Bwana huziongoza hatua zake. Mama Anna aliishi katika
Imani yake thabiti huku akiwa akifanya matendo ya huruma ; nyumba yake ilikuwa
ni nyumba ya mayatima , nyumba ya wahitaji; alikuwa anatimiza ili amri kubwa ya
kumpenda Mungu na jirani: aliishi kwa Imani na uaminifu ule
uliokuwa unampendeza Mungu wetu: hii ni njia pekee ambayo itatusaidia sisi
kujihakikishia, uzima wa milele na furaha ya milele tukikumbuka kuwa yeye ni
tegemeo letu na kimbilio letu; yeye ni kielelezo cha msamaha katika
maisha yetu tunayoishi hapa dunia ikiwa ni sehemu ya safari ya milele;
Upedo sio maana yake tu kupenda lakini ina maana kubwa zidi ya
kuweza kuweka vipao mbele vyako katika kumpenda Mungu na kumpenda jirani. Kama
kama utaweza kufanikiwa katika hili ndipo imani yako, matumaini upendo wa kweli
utakuwa unatwala maisha yako 1 Wakoritho 13:13 Jambo ambalo wengi wanaweza
kujifunza kutoka kwako hasa baada ya maisha ya hapa dunia ni kupima je vita
yako ya imani uliipiganaje? Ulitimiza makukumu yako kama Kristo alivyoagiza
katika mafundisho yake? Yohana 13:34 na 2 Timotheo 4:7.
Mama Anna
alikuwa tayari yeye asiwe na kitu lakini Jirani yake aweze kula na kushiba au
kuvaa vizuri; daiama aliyafanya hayo kwa matendo na mafundisho; daima alikuwa
akitufundisha jinsi ya kuishi kwa upendo na mashirikiano mazuri; kwa msingi huu
yeye na Mume wake Marehemu Mzee Alois waliweza saidia watu wengi sana kwa
kuwajengea misingi mizuri ya shule; waliweza kuishi na watoto wengi ambao
hakuwa na uwezo wa kwenda shule bali wao waliwachukua na kuishi nao kama watoto
wa familia moja.
Je wewe
na mimi tukifa tutacha nini cha kujifunza kwa watoto wetu na jumuia
inayotuzunguka? Je kile tutakacho kiacha kitakuwa kimejaa , upendo, matumaini
na imani? Kama vile mtume Paulo alivyo waambia watu wakoritho fanyeni kila kitu
katika upendo wa Kristo; kwa hiyo; urithi ulio bora hauwezi kupatika kama
hatutamwogopa Mungu; amebarikiwa mtu Yule ambaye anamwogopa Mungu na kutumainia
njia zake na amri zake; Zaburi ya 112:1-2. Tukumbuke kuwa kizazi cha wamuuchao
bwana kitabarikiwa.
Mama Anna aliweza kufuata mfano wa Yesu; Tunajua kuwa Yesu alikuwa
mtu maarufu sana; sio tu kwa sababu aliwalisha wale watu elfu tano pale
mlimani, au alifanya miujiza mingi na kuwaponya wengi; au kwa sababu alikuwa
Bwana wa Mungu; bali alikuwa na vitu vingine vingi ambavyo viliweza kuendana
kabisa na maisha ya sisi binadamu wa kawaida; Yesu alikuwa akiwahudumia watu
wote kwa utu na ubinadamu; mfano tu mdogo wakati ule kule Yerusalemu wasamaria
na wanawake walikuwa wakionekana kama daraja la pili watu ambao hawana thamani
katika jamii yao. Lakini Yesu aliwa hudumia wote sawa kabisa sawa na wayahudi
wengine;
Yesu
alikuwa msikilizaji mzuri; tunatakiwa kujifunza kuwa wasikilizaji wazuri; na
hiyo inasaidia kujua shida na jinsi ya kusaidia kwa urahisi, kwani tutakuwa
katika nafasi nzuri ya kusaidia. Yesu alikuwa sio mtu wa kukimbilia kuhukumu
wengine alikuwa akiongea nao na kuwaelimisha daima alikuwa kama kiongozi
na rafiki; Yesu alikuwa akipatikana kwa urahisi bila masharti au ukiritimba
wowote, mtu yeyote ambaye alitamani kuongea naye alipata nafasi ya kuongea naye,
na hata Yule ambaye alikuwa hawezi kuongea naye kwa sababu yeyote ile aliweza
pia hata kwa kumwita tu akiwa akipita na wengi walipata msaada waliokuwa
wakihitaji. Hakuwa na masharti yeyote hivyo ndivyo alivyokuwa Mama Anna aliweza
kuwa karibu na kila mtu bila kujali khali yake. Jukumu kubwa ambalo liko mbele
yetu tunatakiwa kuendelea kuwa makini katika matendo yetu juu ya Mungu wetu;
tukumbuke kuwa tunaokolewa kwa neema na kamwe kwa nguvu zetu wenjewe; Waefeso
2:8
Nilichojifunza katika maisha ya Mama Yangu katika uhai wake wote
ni Upendo wake kwa kila mtu, Imani yake ambayo haikuyumba kwa wakati wote wa
maisha yake, imani ya kumpenda Mungu, na kuishi kulingana na mafundisho ya Yesu
na kumtumikia kwa moyo wake wote; hata pale alipotukanwa au kudharauliwa kamwe
hakufanya kiburi wala kinyongo; nilichojifunza kwake kama Mithali 22:6 leo
mtoto katika njia impasayo, naye hataiacha hata atakapo kuwa mazee; ilikuwa ni
wajibu wake mkubwa kwetu ilikuwa kuturisisha umuhimu wa imani; kwetu sote na
kumtanganza Kristo kupitia amri kuu ya Upendo; muhimu zaidi amekuwa Mama ambaye
ameishi sana katika ukweli na ameweza kupata thawabu ya kweli kabisa mwisho wa
safari yake hapa duniani; Wafilipi 2: 16 mkishika neno la uzima, nipate sababu
ya kuona fahari katika siku ya kristo, ya kuwa sikujitaabisha bure;
Mama Ana hakuwa anategemea sifa za kupendwa kutoka kwa wanadamu
bali alikuwa akitegemea sifa kutoka kwa Mungu. Alikuwa ni mtu Yule,aliyependa
kutoa zaidi kuliko kutegemea kupata zaidi; alikuwa akitekeleza zaidi amri ya
upendo na kuamini kuwa maisha yake lazima ayatoe kwa watu wengine wanaomzunguka
na ambao wanamahitaji msaada zaidi;
Mama
Anna alikuwa mama Mwema; ambaye daima alikuwa akizungukwa na tabasamu la
upendo; pamoja na mapungufu ya kibinadamu bali alijitahidi kuishi maisha ya
kutimiza amri ya upendo; alikuwa Mama ambaye daima hakujikweza bali
alikwezwa kwa matendo yake; maishani mwake alitamamni kila mtu aishi maisha ya
upendo na kuwajali wengine; Mama Anna hukua tayari kuona unaishi maisha mabaya
ya kumchukiza Mungu; alikuwa msahauri wa mabadiliko; alitamamni sote tuishi wa
upendo kama Yesu alivyofundisha; na alitamani sote tutekeleza majukumu ya
upendo yanayompendeza Mungu hapa duniani.
Alikuwa Mama wa kawaida tu; na daima alikuwa akitosheka na kile
ambacho alikuwa akipata; Alikuwa na Mama ambaye alikuwa akiishi kwa kuwaMfano
Bora wa wa mkiristo anavyopasa aishi; alitosheka na maisha ya kawaida ambayo
yampendezayo Mungu; Mama ambaye aliyatoa maisha yake sadaka ya uwakilishi wa
kweli kwetu sisi kujifunza. Aliitambua imani,alitembea katika imani; alikuwa
Mwamba katika imani yake; alitembea na Mungu ndio maana leo hii Mwenyezi Mungu
amempumzisha kwa amani kabisa; nasi leo tunakila sababu ya kumwita mbarikiwa
kwani amepata kifo chema kilichompendeza Mungu;
AMA KWELI
MAMA ANNA KINUNDA(MBUYA) AMEKUWA DARAJA LA TABASAMU, UPENDO NA MATUMAINI LILILO
MALIZA KAZI KWA USHINDI;
Raha ya
milele mpe bwana na mwanga wa milele umwangazie apumzike katika usingizi wa
Amani na wa ufufuo wa Mungu;
Amina
AMINA Amina
Emmanuel Turuka
2017
No comments:
Post a Comment