·
KWA MOYO WA SHUKRANI NA UNYENYEKEVU?
·
KWA MOYO WA MALALAMIKO?
Katika
kipindi hiki cha Kwaresma tafakari yetu ya wiki hii inatuuliza swali moja je
sisi ni watu wa kushukuru au ni watu ambao tumejaa malalamiko tunavyoyakabili
maisha yetu ya kila siku?
Tujikumbushe
kuwa Mungu wetu ni Mungu aliyejaa huruma na ni Mungu ambaye ni mtoaji; lakini
sisi kama wana wake je tunatambua ukuu wa mungu katika maisha yetu? Je zawadi
zote ambazo Mwenyezi Mungu anatujalia sisi tunazipokeaje, tunazipokea kwa moyo
uliojaa shukrani au tunazipokea kwa kuturidhika na kwa malalamiko? Tatizo letu
tunasahau haraka sana zawadi ambazo Mungu anatujalia katika maisha yetu, na
daima tunaishia kuwa watu ambao tunakuwa wa kulalamika zaidi na sio kushukuru
na kuomba bila kuchoka.
Lakini
tunabahati kubwa pamoja na malalmiko yetu Mwenyezi Mungu bado anaendelea
kutupenda na kutujalia sisi mahitaji yetu. Tukumbuke jinsi wana wa Israeli
walivyokuwa wakilalamika lakini kila siku mpya Mwenyezi Mungu aliendelea
kuwalinda na kuwapa mahitaji ambayo walikuwa wakihitaji kwa siku hiyo.
Katika kipindi
hiki cha Kwaresima tuendelee kufunga na kusali tukiomba msamaha kwa kosa hili
kubwa la kulalamika hata pale tunapotendewa mema. Tunatakiwa kupokea kila
zawadi tunayojaliwa katika mikono ya shukrani.
Tukumbuke kuwa mbele ya Mungu malalamishi sio kitu cha kujivunia. Unyenyekevu,
moyo wa shukrani ndio vitu vya kujivunia mbele ya wenzetu na Mungu.
Tukumbuke
kuwa wakati mwingine Mungu anatupa sisi zawadi ambazo hatustahili kabisa. Je
kuna zawadi gani kuwa zaidi ya Kumtoa mwanaye aje ulimwenguni ateseke na kufa
kifo cha aibu kwa ajili ya dhambi zetu ili sisi nasi tufurahie utukufu wa Mungu
Mbinguni. Kwa kuja kwake sisi tumekombolewa.
Tunavyo
kumbuka mateso ya Yesu, tujikumbushe kuwa mateso yake yamekuwa ufunguo ambao
umetufungulia sisi uzima wa milele. Yesu ameweza kutusaidia sisi kukata kiu ya
kufurahia maisha maisha yetu ya baadae; kwani tukiweza kuishi ndani yake kwa
matendo kamwe hatuwezi kuogopa kifo; kwani uchungu na ugumu wa Kifo Yesu
ameshauondoa.
Kwaresima
hii itukumbusha kuwa Yesu ndio mkate kweli wa uzima ambao unasafisha kabisa
njaa, wajibu wetu ni kuendelea kuishi kulingana na mafundisho yake. Na kubwa
ambalo tunakumbushwa leo tuache kulalamika bali tupokee zawadi zote tunazopewa
kwa upendo na kwa moyo wa shukrani ili neema ya mungu ibaki juu yetu.
Ili kuweza
kuijiimarisha katika zawadi hii Yesu anataka sisi leo kuendelea kujifunza
umuhimu wa zawadi zote ambazo tunazipata leo kupitia watumishi wake ambao
wamepewa uwezo wa uwakilishi wa Kristo katika maisha yetu. Wao ni binadamu kama
sisi bali ni chombo kilichobarikiwa katika kutekeleza mafundisho ya
kutuelimisha sisi umuhimu wa kupokea zawadi zetu kwa moyo mkunjufu uliojaa
upendo na shukrani na sio kujijengea tabia ya kulalamika na kuona kuwa Mungu anatuchukia;
Tukiweza
kupokea zawadi hii ndipo tunapotambua ukuu wa neema ya mungu juu yetu; Mungu anatujenga
sisi katika imani kubwa kama tutaweza kuacha kabisa malalamiko, tutakuwa
tumekomaa katika imani. Katika tafakari yetu ya wiki hii tumpe asante mungu kwa
upendo wetu kwetu kwa kutujalia sisi ridhiki yetu ya kila siku na tunamshukuru
kwa kutujalia sisi pia mkate wa uzima jambo la msingi ambalo ndilo linalotawala
tafakari yetu je sisi tunapokeaje hii zawadi kubwa ya ukombozi wa maisha yetu?
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment