November
1 wakorinto. 12.13
Tafakari ya neno kubalikiwa lina maana
pana na sio ile ambayo imezoeleka ya kufurahia mafanikio au raha hasa za
kimaisha yetu ya kila siku; na mara nyingi tunafurahi sana tunapofanikiwa
katika maisha yetu na hapo kwa sauti ya juu tunaimba na kushukuru kuwa
tumebarikiwa; wote tunahitaji kubarikiwa na kufurahaia maisha yetu ya kila siku
katika ubora wake wa khali ya juu. Nami najua kabisa hakuna mtu hata mmoja katika
misha yetu ya kila siku ambaye hukataa maisha mazuri ya Baraka.
Tafakari yetu inatukumbusha kuwa mara
nyingi tunapoangalia kubarikiwa tatizo letu tunaangalia Baraka katika upande
tofauti nap engine kwa namna ya pekee; tukiangalia kuwa Baraka asili yake
mafanikio ya asili; kwa msingi huu pale tunapokaa kwenye nyumba nzuri, kazi
nzuri,gari nzuri na kadhalika kwetu tunajiona kuwa tumebarikiwa na tunafurahia
sana na tunaimba aleluya kwa Mungu ametubariki; warumi , 8:17 na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na
Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye.
Tafakari yetu inataka tujiulize je pale inapotokea pengine
tunaumwa; au unaendesha gari ambalo sio nzuri au unaishi katika nyumba ambayo
sio nzuri; je hapo tumekuwa tumepoteza Baraka za Mungu? Au pale maisha
yanapokuwa magumu ha uwezo wa kifedha umeondoka na hatuwezi kuyakabili msiaha
kwa ujumla je hapo Baraka za Mungu ziko wapi? Nafikiri kuwa tatizo letu
tunaangalia Baraka katika mwelekeo mmoja tu wa mafanikio na sio shida; katika
mwelekeo huu wa kuwaza kutumbuke kuwa Gari linaweza toweka siku moja, pesa
zinaweza toweka siku moja, hivi vitu vyote ambavyo tunavyoviona katika macho ya
kidunia ni njia ya kutusaidia sisi ili tuweze kuzifikia barka za Mungu katika
ukamilifu wake; tujue kuwa hivyo vyote ni vya muda tu lakini Baraka na neema za
Mungu ni za kudumu. Hata afya yetu siku moja itaporomoka na hatutaweza irudisha
tena; hivyo tunatakiwa kufahamu kuwa Baraka
za kweli sio mali ni vyote vinavyotuzunguka bali baraka ya kweli ni roho wa
Mungu ndani yetu; Warumi 8:28-31 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi
pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa
kusudi lake. Maana
wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa
Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi. Na wale aliowachagua tangu
asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia
haki, hao akawatukuza. Basi,
tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
Tafakari yetu inaendelea kusisitiza kuwa Je ni furaha ya namna
gani pale ambapo vyote vimetoweka lakini bado unaendelea kumiliki Baraka za
Mungu , hivyo ni wajibu wetu sasa kutambua Baraka za Mungu ndani ya Maisha
yetu; halafu kitu ambacho tunatakiwa tujivunie ni utambuzi kuwa tayari Mungu
ameshatujalia Baraka katika maisha yetu; katika wakati uliopita ,wakati wa sasa
na wakati wa baadae;lakini Mungu ametupa sisi vitu vyote vya kutupatia na
kutuongoza kuishi katika Baraka zake, ili tuweze kuwa washindi, ili kutusaidia
kuwa watiifu, na kuwa na thamani katika maisha ya Kimungu katika ufalme wake;
Tafakari yetu tukisoma Waefeso 2:12, kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya
Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna
Mungu duniani. tukumbuke kuwa
tumepata kibali cha baba na tumelelewa
kwa damu ya Yesu; hivyo njia pekee za kufurahia Baraka za Mungu lazima
tuuishi wokovu na neema ya Mungu itubariki, hivyo tunatakiwa tuziangalie Baraka
zetu kutoka katika mpangilkio na mwelekeo wa Kimungu; hapa tutaweza kutambua
kuwa kila kitu ambacho kipo mbele yetu kimebarikiwa kweli kweli; hapo
tutatambua kuwa Mwenyezi Mungu ametubariki sisi san asana ambazo hazipimiki
hivyo wajibu wetu ni sisi kumshukuru Mungu kwa Baraka hizo hata kama
tunakabiliwa na matatizo mengi ya maisha lakini wajibu wetu ni kumshukuru na
kumsifu Mungu kwa Baraka zake juu yetu .
Hii ndio tafakari yetu ya leo Amina
Emmanuel Turuka
No comments:
Post a Comment