NOVEMBER
Tafakari yetu leo
tujikumbushe ujumbe huu mzuri kuwa kama una imani mlango wa matumaini
utafunguliwa dhidi yako; tunajua kuwa maisha yetu hayajejengwa katika mstari
ulionyoka ambao sisi tunatembea tukiwa huru; bali ni safari ambayo huwa ina
vikwazo, vigugumizi, mabonde, milima na mapingamizi ambayo tuwapo safarini lazima tuwe tayari
kukabiliana navyo, na urahisi wa kushinda vikwazo hivi ni kuwa na imani
inayotakiwa. Hivyo tukiwa na imani tuwe na uhakika kuwa mlango utafunguliwa;
Tafakari yetu inatufundisha huu ukweli ambao haupingiki
kuwa kujifunza tofauti kati ya imani na kuamaini ni kitu ambacho tunatakiwa
kukifanya kila siku katika maisha yetu yote; ndio maana mafundisho
yanatukumbusha kuwa Mungu anapenda sisi
tumwamini yeye kwa akili zetu na kwa dhamira zetu bila shuruti; na tutaweza
kumwamini yeye kwa matendo yetu na katika shida zetu; tukiamini kuwa yeye pekee
ndiye kimbilio letu katika mahitaji yetu;
Tafakari
inatukumbusha kuwa matumaini na kumwamini mungu lazima yaanzie kwetu kupitia
maombi yetu ya kusifu na kushukuru; Tumkumbuke Ayubu pamaoja na shida na
magonjwa aliendelea kumtumaini Mungu na Mungu alimbariki; Kama ilivyotokea kwa
Ayubu nasi tumaini letu katika mahangaiko yetu ni imani na matumaini makubwa ambayo tunatakiwa
tuyatangulize mbele ya Mungu, kwa kufanya hivyo Mungu hufunga mlango wa mateso
na kwa kweli huwa hauana faida na maisha yetu na kukufungulia Mlango mwingine
ambao umejaa matumaini; Mungu huonyesha njia kupitia mlango ambao umefungwa na
ule ambao anaufungua kwa ajili maisha yetu; Mwenyezi Mungu anapofunga mlango
mmoja anataka wewe ubadilisha mwelekeo wako wa maisha; na unavyobadilisha
mwenendo wako wa maisha na ili uweze kutembea katika mafanikio na neema ya
utukufu wako kupitia mlango mpya alioufungua kwako;
Tafakari
yetu inatukumbusha kuwa tatizo letu mara nyingi tunajikwaa katika barabara
yenye makorongo ambayo imetengenezwa kwa lami ambayo imejaa mashaka na kukosa
imani; lakini mwenyezi Mungu daima hututembeza katika barabara iliyo imara na
bora yenye imani kubwa ambayo hutuongoza sisi katika mlango ambao umejaa matumaini
na kutufungulia mlango ambao hatukuutegemea kabisa; mungu wakati mwingine hata
hatuambia kuwa tuende kushoto au kulia yeye anachofanya ni kufunga mlango ambao
hauna faida kwetu na kutufungulia mlango ambao umejaa neema. Hivyo wakati
mwingi mlango ukifungwa ni neema vile vile.
Tafakari tunatakiwa
tuendelee kushukuru hata tukiwa kazini tunapopatwa na mitiani mbalimbali iyojaa fitina, chuki na kadhalika mshukuru
Mungu kwani kuna neema kubwa inakuja mbele yako. Tukumbuke kuwa Mungu
anayaendesha maisha yetu upendo wake hufunga na kufungua milango ya kuingia na
kutoka katika maisha yetu; Tunajua kuwa inakuwa ngumu katika ubinadamu
kulikubali na kulishukuru hilo mara moja. Tukumbuke kuwa Daima Mungu anatemebea
mbele yetu, anajua mapito yetu kabla sisi hatujeyajua yeye ni kinga yetu ya
kweli; ndio maana siku zote tukiwa na imani hutuepusha na mabaya yote mbele
yetu; lakini kwa sababu ya kukosa kwetu hekima sisi tunajiona kuwa tunajua na
kumsukuma pembeni lakini baada ya kumsukuma na kupata matatizo tunarudi na
kuanza kumlilia huku tukimlalamikia sana kwa nini umenifanyia hivi na hivi.
Tafakari
yetu leo inatukumbusha kuwa tunapopatwa na tatizo kwa kiwango chochote kila
Mungu tayari anakuwa ameshajua tatizo na suluhisho lake; anachohitaji kutoka
kwetu ni sisi kumwamini yeye na kutekeleza sehemu yetu ambayo ni maisha
kulingana na maagizo yake; na jukumu letu nyingine ni kuendelea kusali na
kumshukuru; na tukumbuke kuwa tutafanikiwa kwa kusoma vitabu vyake na kuamini
kuwa yeye ndiye suluhisho la matatizo yetu yote:
Hii ndio
tafakari yetu ya leo tumtumaini mungu katika njia zake na katika maamuzi yake
kwetu ili tuendelee kupokea Baraka zake bila kikomo. Amina
Emmanuel
Turuka
No comments:
Post a Comment