WELCOME - KARIBUNI SANA

GOD’S PROMISES ARE NEW EVERY MORNING” LAMENTATION 3;23

“All our dreams can come true – if we have the courage to pursue them.” - Walt Disney


Saturday, May 14, 2016

WEMA NA FADHILI ZA BWANA

May 14

Tafakari ya leo tujikumbushe wema na fadhili za Mungu ambazo zimeendelea kutuzunguka kila siku katika maisha yetu. Sisi tumepata bahati ya kubwa ya ufadhili na upendeleo wa  Mungu katika kila hatua ya maisha yetu.

Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa pale ambapo tumekuwa tukikosea bado kwa upendo na  neema yake tumekuwa tukipata msamaha wa makosa yetu.

Tafakari yetu vile vile inatufundisha jinsi ambavyo kwa upendo wake alimtoa kwetu bwana wetu Yesu Kristu awe kimbilio letu na ondoleo la dhambi zetu. Damu yake iliyomwagika msalabani alipokufa katika kifo cha msalaba imetupa sisi ushindi wa ajabu sana.

Tunakila sababu ya kutembea kifua mbele kwani wema wake unaendelea kutuzunguka daima. Wema wake  hauna mipaka,  wema wake ufunguo wa maisha yetu  katika safari yetu ya mbinguni.

Tuna kila sababu ya kushukuru na kusema Aleluya. Ni wajibu wetu sasa kumpa Mungu shangwe zetu bila kukoma. Amina

Emmanuel Turuka

Friday, May 13, 2016

BWANA YESU NAKUPENDA

MAY 13 

Tafakari ya leo tumshukuru Mungu kwa upendo wake kwetu kwa ukombozi wa Bwana wetu yesu kristo. Yeye alitupenda sana na kutufia msalabani  tunakila sababu ya kumpenda. asante Yesu kwa upendo wako.

Thursday, May 12, 2016

TUNAHITAJI WAZO LILILO SAHIHI



May 12

Tafakari Ya Leo Tuangalie Nguvu Ya wazo Katika Maisha yetu. Tukumbuke kuwa maisha yetu yamejengwa na  wazo. Wazo  ni  zao  la kazi  ya  akili ambayo  inaleta fikra juu  jambo  au  khali fulani. Wazo huzaa  neno- kupitia neno  akili yetu hutafuta njia  ya  kuelezea wazo. Ili  neno liweze kutimiza haja hugeuka kuwa kielelezo cha wazo - neno  ili liweze kuonekana kupitia kigezo. (Concept ).
Tafakari yetu leo inatukumbusha kuwa wazo ambalo hugeuka kuwa neno lazima lielezwe kupitia, mawasiliano  (communication). Mawasiliano ili yaweze kufanya kazi lazima yawe ya pande mbili. Pande hizi zinaweza kukubaliana au kutofautiana.

Wednesday, May 11, 2016

HATUJECHELEWA MUNGU KUSAFISHA UCHAFU WETU




May 11

Tafakari ya leo inatukumbusha kuwa pamoja na uchafu wote ambao tunao katika maisha yetu, ni wazi kabisa hakuna sabuni yeyote ambayo inaweza kutusafisha na  uchafu huo. Sabuni pekee ni  damu  ya  Yesu.  Mkumbuke Daudi  alivyomlilia Mungu baada ya  kufanya dhambi ya kuua, ili kufanikisha adhama yake ya kuhahalisha uchafu wa zinaa.

Sisi leo tunafanya uchafu wa kila aina na  kujisifu kuwa nguvu yetu ya kibinadamu ina nguvu kuliko nguvu ya Mungu. Kwa kweli tunajidanganya sana. Uchafu ambao umezunguka mwili wetu, unatoka na na  kiburi chetu, na kujiona kuwa sisi tuna  akili ziadi ya Mumgu, afya njema ambayo tunayo ni haki yetu na haina uhusiano wowote na upendo wa Mungu; Lakini tunatakiwa kukumbuka kuwa hata   nguvu ni sehemu ya upendo wake kwetu ili tuweze kutimiza mahitaji yetu kulingana na mwongozo wake.

Leo hii sisi tumekuwa wale wanaoendesha Gari huku tukitazama nyuma,  hivyo hatuko tayari kwa ufalme wa Mungu. Tunatakiwa kufuata maelekezo na mafundisho ya bibilia ili tuweze kutembea katika njia ya bwana inavyotakiwa tutembee;


Siku ya  leo  tujitafakari kuwa hatujechelewa kusafisha uchafu wetu,  kwa sharti moja, la kumkabidhi Mungu maisha yetu kwa dhati na kuishi kulingana na sheria zake. tukitimiza ili amri kuu ya upendo na kuishi kwa vitendo - Amina

Tuesday, May 10, 2016

TAFAKARI UPENDO WA MUNGU

May 10


Tafakari yetu tuendelee kushukuru upendo wa Mungu na jinsi anavyotupenda wanadamu.

Sunday, May 8, 2016

SIKU YA KUMBUKUMBU YA KUSHEREKEA KIUNGO KIKUBWA CHA FAMILIA- MOTHERS'S DAY



May 8

Mithali 14; 1

Tafakari ya leo tunakumbuka kiungo kikubwa sana cha  familia yetu. Siku ya  kuwaenzi akina mama wote Duniani.  Tukumbuke kuwa mchango  wa  mama zetu na akina mama  wote  ni  mkubwa katika makuzi ya familia. Familia  ni  kielelezo cha juu kabisa cha  jamii yetu. Tukumbuke kuwa jamii ni  zao la familia.  kielelezo cha  familia zetu hakiwezi kukamilika kama hatutaenzi wajibu wa mama  ndani  ya  familia.  Kama  kitabu cha mithali 11- 6 kinavyosema Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata    heshima, Apataye mke apata kitu chema  naye ajipatia kibali kwa BWANA;huu ni ukweli mtupu ndio maana tuna kila sababu ya kusema asante sana kwa upendo wenu huo. 

Je umuhimu wa mama katika familia umejikita zaidi katika malezi? Jibu la  swali Hilo ni  hapana.  Wajibu wa  mama pamoja na ukuu wao katika malezi kwa  kweli wamevuka mipaka.  Ndio maana waswahili hunena kwenye mafanikio makubwa ya  mwanaume yeyote nyuma yake kuna  nguvu ya  mwanamke. Kama Mtaalam mmoja aliwahi sema kuwa  pindi mtoto anapozaliwa na mama anazaliwa pia, mama hakuishi kabla; bali mwanamke anaishi muda wote lakini mama ni kitu kipya kinachokuja baada ya mtoto kuzaliwa;lakini ndio wajenzi wakuu wa familia Mithali 14; 1 inatutaadhalisha kuwa Mwanamke mwenye hekima huijenga   nyumba yake,  bali mpumbavu huibomoa nyumba yake    kwa mikono yake mwenyewe.

Tafakari yetu Leo siku ya kuwashukuru sana  “ Mama” kwa jinsi wanavyojitolea katika kuhakisha kuwa kila kitu ndani ya familia kinakwenda vizuri, kama mama ni legelege ndani ya familia na familia itayumba tu; Ni ukweli usiopingika kuwa katika kila mafanikio makubwa ndani ya familia nyuma yake yuko Mama; Mitahali 5- 18 inaendelea kutufundisha kuwa Chemchemi yako na ibarikiwe  na ufurahie mke wa ujana wako;

Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuwajalieni busara, upendo, ujasili na unyenyekevu ambao ni daraja la msingi sana katika kuimarisha nyumba bora yenye upendo mkubwa. Kwa namna ya pekee leo napenda kuwakumbuka na kuwashukuru sana na nazidi kumwomba Mungu azidi kuwajalia afya njema na amani katika maisha yenu ya kila siku hii ya kumbukumbu yenu mmekuwa daima kiungo muhimu sana katika maisha yetu na katika ukuaji wa familia. Hekima yenu haina mipaka, upendo wenu hauna mipaka, msamaha wenu hauna mipaka; nasi tunaendelea kumshukuru Mungu katika kuenzi ukuu na ujenzi wa familia zetu;

hii ndio tafakari yetu ya leo Amina

Emmanuel Turuka