Nilikuwa natafakari kuhusu dhana nzima ya ujumbe huu wa kumwomba bwana akae nasi kwani jua linatua. Nimejiuliza maswali mengi ya kisalfasa. Kwa nini tumwombe Mungu akae nasi. Kwa nini tusiwaombe watu mashuhuri, wenye akili nyingi? Watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha ambao dunia inawaheshimu. Kwa nini tusiwa ombe watu mashuhuri ambao wanaongoza madhehebu tofauti ambao Wana nguvu katika dunia hii? Wasiwasi wetu unatokana na nini wakati jua linatua? Kuna siri gani kati ya jua kutua na kuomba Masada wa Mungu?
Kwa nini tunakuwa wepesi wa kumkimbilia Mungu katika mashaka yetu, na wakati wa furaha tunasahau uwepo na nguvu ya Mungu?
Kwa nini bado tunawsogopa na kuwajali wenye pesa na kusahau kuwa bila uhai ambao unatoka kwa Mungu hawa wote tunawaona muhimu katika dunia hii Si chochote.
Hii ni tafakari katika siku ya Leo, je wewe ni miongoni wa wanaokimbilia Masada na huruma ya Mungu? Au wanaokimbilia watu maarufu katika dunia hii.
Basi kama jibu ni ndio kimbilia huruma ya Mungu na Mungu atakaa nawe wakati jua likitua. Amina
No comments:
Post a Comment