Kumsamehe yule aliyekutendea yasiyo sahihi hutusaidia
kutupatanisha na Muumba wetu; vile vile msamaha hudumisha mshikamano wa udugu
ambao umeharibiwa. Kwa kusamehe tunaandaa njia ya kumwendea Mungu; Lakini pasipo imani
haiwezekani (Waebrania 11:6).
Inatufundisha kuwa mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini
kwamba yeye yuko,
na kwamba huwapa
thawabu wale wamtafutao,”. Msamaha hutujengea wa kumwendea na Kuishi na
Mungu katika Imani.
Kama ilivyoandikwa hakuna mwenye haki, hata
mmoja” (Warumi 3:10). Mungu yuko tayari na anasubiri kumsamehe mtu anaye omba
msamaha imeelezwa katika Zaburi 86:5 "Kama wewe Bwana u mwema, umekuwa
tayari kusamehe, na mwingi wa fadhili kwa watu wote wakuitao". Daudi
aliweka wapi tumaini lake la msamaha? Tukisoma Zaburi 51:1 "Ee Mungu
unirehemu sawasawa na fadhili zako kiasi cha wingi wa rehema zako uyafute
makosa yangu. Mathayo 6:14-15 Kwa maana
mkiwasamehe watu makosa yao na Baba wenu wa mbinguni atawasamehe ninyi bali
msipowasamehe watu makosa yao wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu."
Wale wamesamehewa husamehe. imeandikwa Waefeso 4:32 "Tena iweni wafadhili
ninyi kwa ninyi, wenye huruma ninyi mkasameheane kama na Mungu katika kristo
alivyowasamehe ninyi."
Kusamehe kwa kweli
hakuhesabu makosa. imeandikwa Mathayo 18:21-22 "Kisha petero akamwendea
akamwambia Bwana ndugu yangu anikose mara ngapi nami ni msamehe? hata mara
saba? Yesu akamwambia sikwambii mara saba bali hata saba mara sabini."
Katika kusamehe Yesu ametukomboa kutoka kwa dhambi na mshahara wa dhambi.
Wakolosai 2:13-14 inatueleza kuwa "Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu
ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu aliwafanya hai pamoja naye
akisha kutusamehe makosa yote akisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya
kutushitaki kwa hukumu zake iliyo kuwa na uwadui kwetu akiondoa isiwepo tena
akaigongomea msalabani."
Zaburi 51:7-12
"Unisamehe nami nitakuwa safi, unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko dheluji
unifanye kusikia furaha na shangwe, mifupa ilio ponda ifurahi. usitiri uso wako
usitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi
uifanye upya roho iliyo tulia ndani yangu usinitenge na uso wako wala roho wako
mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wakovu wako unitegemeze kwa roho
ya wepesi."
Zaburi 32:1-6
"Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake heri Bwana
asiyemhesabia upotovu, ambaye rohoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa
yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa na kwa maana mchana na usiku
mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawa kama nchi kavu wakati
wa kaskazi nalikujulisha dhambi yangu wala sikuuficha upotovu wangu nalisema
nitayari maasi yangu kwa Bwana naweukanisamehe uoptovu wa dhambi yangu kwa hiyo
kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu yafurikapo
hayatamfikia yeye."
Wale walio
wanyonge moyo wako mbele ya Mungu na wala kutambua hatia yangu, haijafika hali
ya kwanza ya kukubalika. Tunahitaji kuokolewa kutoka katika aina zote za tabia
zetu mbaya pamoja na misukumo ya ndani inayotushurutisha kufanya mambo fulani
mabaya: kama vile, kusema uongo, hasira inayomfanya mtu atukane watu, tamaa
mbaya za mwili, uchungu, kutaja machache tu.
Hatuwezi kujiokoa
wenyewe kutoka katika dhambi au kuigeuza tabia yetu kwa kujitegemea wenyewe
kama vile Simba asivyoweza kuamua awe mwana-kondoo (Warumi 7:18). Dhambi ina
nguvu nyingi kuliko nia yetu ya kufanya yale tuyatakayo. Lakini Kristo anaweza
kukufanya wewe uwe "imara kwa uweza wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu
[wako] wa ndani" (Waefeso 3:16). Anafanya kazi yake ili kuondoa tabia zetu
ziletazo uharibifu na mahali pake kuweka tabia hizi nzuri: upendo, amani,
furaha, upole, uwezo wa kujitawala (Wagalatia 5:22,23). Kristo anaishi maisha
yake kupitia ndani yetu, kisha tunapokea uponyaji wa kiroho, tunarejeshwa
katika maisha mapya, na kuwezeshwa kuishi maisha hayo mapya.
Hakuna dhambi
ambayo ni ya kutisha sana asiyoweza kuisameka Yesu anatamani sana kwamba kila
mmoja wetu hatimaye awe na uhusiano mzuri na Yule aliyemkosea na kumsababishia
majeraha ambayo yamejenga chuki ambayo inahitaji msamaha. Yesu anataka tupokea
msamaha na utakaso wa Mungu ni; katika
imani jambo ni rahisi na la maana
sana kama tunavyofurahia kumpokea motto mdogo aliyezaliwa na kumkumbatia.
Lakini kutokana na ubinadamu wetu, majivuno, kiburi, masengenyo inatuwia vigumu
sana kutoa msamaha wa kweli pale tunapokosewa, tunakuwa na kiburi ambacho
kinatufanya kuona kuwa Yule aliyetukosea hastaili msamaha wetu; lakini kama
tunayafuata mafundisho ya yesu na mifano ambayo ametutolea katika Bibilia
Takatitifu tunatakiwa tuondoe ugumu katika mioyo yetu na kuuvaa unyenyekevu
kama yeye alivyovaa unyenyekevu na kuuvua Umungu kwa ajili ya makosa yetu, na
alikuja kukaa nasi na ametutengenezea daraja la msamaha ambalo kila mwanadamu
lazima alipite ili kuweza kukamilisha safari yake ya kwenda mbingu.
No comments:
Post a Comment