JANUARY 18: 2019
WAEBRANIA 11:6
WAFILIPI 4:12-13
WAKATI WA MASHAKA IMANI THABITI INAHITAJIKA:
Somo letu leo tunakumbushwa kuwa wakati wa mashaka; tabu; wakati ambapo tunakabiliwa na sinto fahamu; tunatakiwa kuendelea kusimam imara kumwamini Mungu kama zaburi ya 23 inavyotukumbusha.
Imani iliyojaa Matendo Ndio iwe kimbilio letu kwa Mungu na tukumbuke Mungu hutenda Kazi ndani ya wote wanao matumaini kwa imani wakati wowote ule wa maisha Yao:
Imani Yako ijae Matendo na kuamini kwa dhati kuwa Mungu ni mwanzo na mwisho wa kila Jambo katika mazingira yeyote yale:
Tujifunze hili Imani tunapoitenda kwa Matendo yatupasa kuhakikisha kuwa pasiwepo yeyote wa kumwamini zaidi ya Nguvu ya Mungu:
Tumeona katika simulizi mbalimbali wale wote waliokubali kutembea kwenye kasi ya imani kwa kumtegemea Mungu walifanikiwa sana.
Jiulize wewe sasa,ni nini kinachokupunguzia mwendo kasi wa kuamini katika imani na kufuata sheria za Mungu?
Usikubali mtu akupunguzie mwendo kasi wa utekelezaji wa imani yako kwa vitendo: Waebrania 11:6 Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Mfano mzuri ni kutoka kwa Yesu mwenyewe alipata mitihani mingi katika maisha yake ya utumishi: Siku zote alikuwa mshindi kwa sababu alimtumaini Mungu na kuishi kwa kadiri ya mapenzi ya Mungu:
Shida yetu tumekuwa wepesi sio wa kuamini bali kujijengea hofu tunapokabiliwa na Matatizo: Mungu anakuwa sio kimbilio letu:
Hofu; hofu hututawala na kutufanya kukata tamaa mapema: Tuyakumbuke maneno ya Paulo kwa Wafilipi 4:12-13 Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa.
13 Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Tukiwa na Imani yetu thabiti kwa Mungu tutayaweza na kuyashinda yote:
Hili ndilo somo letu la leo Imani sahihi ni msingi wa mafanikio yetu yote:
🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿🙏🏿👏👏👏👏👏
Emmanuel Turuka
Kalamazoo MI 49009
2019